Song: Kumbe Ndivyo ulivyo
Artist:  Rose Muhando
Year: 2021
Viewed: 75 - Published at: 4 years ago

Naona kama maono, kumbe ndivyo ulivyo
Nilidhani 'kama ndoto, kumbe ndivyo ulivyo, Nilifikiri nachanganyikiwa kwa kusema hivi, kumbe ndivyo ulivyo
Umekuwa mpole, umekuwa mwenye huruma, kumbe ndivyo ulivyo ooh
Si mwepesi wa hasira, baba ni mwingi wa rehema, ndivyo ulivyo oh
Wewe unatuwazia mema, kuliko tunavyodhani, ndivyo ulivyo
Mawazo yako hayafanani na mawazo ya wanadamu, baba ndivyo ulivyo
Nani kama wewe, mwepesi wa kusamehe, ndivyo ulivyo ooh
Wema wako hauneneki katikati ya wanadamu Jehova, Kumbe ndivyo ulivyo;

Ndivyo ulivyo, ndivyo ulivyo
Ooh ndivyo ulivyo
Hakuna Kupinga
2)
Tulia kwa Mungu, hushuka na kutufariji, Baba kumbe ndivyo ulivyo oh
Usiku na mchana hulali husinzii Mungu uliye hai, ndivyo ulivyo ooh
Pale tusipoweza kutenda wenyewe kwa mikono yetu Yehova, ndivyo ulivyo ooh
Huingilia kati 'yale yote tunayoshindwa wewe ndivyo ulivyo
Msaada wakati tunapochoka, Yehova
Ndivyo ulivyo ooh;

3)
Mungu uliwakusanya walioachwa
Ukawakumbatia baba ndivyo ulivyo
Waliokosa tumaini weka tumaini jipya kwao, ndivyo ulivyo ooh
Waliokata tamaa, wewe unawatia nguvu baba ndivyo ulivyo ooh
Vile nionavyo mimi si kama utazamavyo baba kumbe ndivyo ulivyo oh
Huruma zako zimevuka vilindi vya bahari, Mungu we eeh kumbe ndivyo ulivyo
Hakuna Kupinga;

( Rose Muhando )
www.ChordsAZ.com

TAGS :