Song: Muscular Feminist
Artist:  Dizasta Vina
Year: 2021
Viewed: 86 - Published at: 2 years ago

Dear boys dear… men

Ni sisi wasichana kina dada, mabinti na mama zenu
Tunaongea kutoka upande wa chini, upande mbali upande kutoka usawa wenu

Upande nilipo msichana kuna hitilafu
‘So’ sikio lako thabiti ni ushindi kwangu
Ninayotaka kusema hapa sio siri katu
Ili ujue nina vingi vya ku-offer kabla ya mwili wangu

Kwa miaka mingi nimeishi gizani
Gizani kwenye baridi na miba mingi nyikani
Eneo uliotaka niishi ni eneo kandamizi
Na bahati mbaya we’ ndo’ mchoraji wa hii ramani

Ramani inamwonyesha binti kama chombo cha mapenzi
Msindikizaji mtoto tegemezi
Ramani isiyojua vituo
Isiyojua tunaweza kuwa marafiki bila kuvuana nguo

Dear boys, dear men
Mngeelewa mngeiweka fikra sahihi
Kama sanaa jinsi inavyozalisha fasihi
Mi’ ni mlezi ukinivika mi’ umeivika jamii

U-gentlemen sio kulipa mgahawani
Umeshapitwa na wakati
Hainisaidii kunifungulia mlango nikifika kwenye gari
Nifungulie fikra nitafakari

Dear boys, dear men

Tumekuwa tegemezi maana mmeficha mbegu
Nani wa kuipigana vita yetu
Umbali kati yetu utakuwa mkubwa milele
Maana si ni wahanga wa mifumo mliyoiunda wenyewe

Nikijaribu kusoma nabaki bure
Maana unajali mwili wangu, ndo’ maana sitaki shule
Kila nikienda popote wanaomba ngono
Labda niwe changudoa to the fullest
At least I’ll get paid

Hata sisi tuna life too
And the world doesn’t revolve around you
Nipo tofauti sikupenda, na tena
Unaponichezea fahamu kuwa ninazeeka mapema
Shujaa unakumbukwa mzazi sikumbukwi
Na kwanini kuwa msafi sio haja kwako
Au kutembea kifua wazi ni kujiamini
Nikitembea mimi ni nusu uchi

I wish ungejua pride yako nayo sumu
I wish ungejua kuwa uanaume sio nguvu
I wish ungejua kuwa binadamu hajakamilika
Mwanaume aliyekamilika anatimiza majukumu

I wish ungejua kuwa na mimba sio haya
I wish ungejua mwanamke kuwa kichwa si vibaya
I wish ungejua kuwa upendo nao una nguvu kwahiyo mwanamke akitongoza mwanaume si malaya

I wish ungejua kuonyesha fear sometimes, it’s okay
It’s okay kulia sometimes
I wish ungejua uongozi hauoni jinsia si
Tatizo mwanamke kuongoza njia sometimes

Mifumo mliyoianzisha ina maisha
Na chenye maisha kinazikwa
Kwahiyo ipo siku mwanamke atasimama
Na vita tunayopigana tutashinda

Inasikitisha hamkui kihisia, japo mnakua kiakili
Natamani … natamani mngejua kuwa inauma sana kuwa namba mbili kwenye kila nyanja
Ego ni power ila iogope
Maana ni upanga unaokata pande zote
Ngoma nzuri ngoma nzuri haitavuma milele
Ukitumia ubabe vibaya utakuvunja mwenyewe

Hadithi ya mwanamke alimshawishi Adam kula tunda
Iliandikwa na wewe
Sijui Delilah alichukua nguvu za mumewe akaziuza
Iliandikwa na wewe

Upande wangu wa hadithi haujasikilizwa
Pengine hautasikilizwa hasirani
Maana ulianzisha shule akasoma mwanaume
Mwanamke nikabaki nyumbani

Dear boys, dear men

Hamtakaa kwenye kilele
Maana kilele ni kuwa mama
Mi’ ni kichwa sio wewe ungekuwa kichwa
Mtaani kusingekuwa na single mothers

Lini mtaacha kutuita mademu
Au labda mwite demu mama’ako
Ukiona hauwezi naomba niheshimu kwa maana heshima inaanza kwako

Na haja ya maelewano iko hapo
I mean… ipi salama ya kichwa cha familia bila
Mkono wa kuosha macho?

Najua tupo tofauti
Na tofauti yetu itabaki, itabakia hivyo milele
Ila naomba usinichukie nielewe

Dear boys, dear men

Ni sisi wasichana, kina dada, mabinti na mama zenu
Tunawasilisha kutoka upande wa chini upande wa pili
Upande mbali kutoka usawa wenu

Dear girls, dear Women

Ni sisi kina kaka, kina baba, wanaume machizi wenu
Tunaongea kutoka upande wa juu, upande wa mbali
Upande uliowekwa na asili yetu

Upande wenye mafungu yenye ulanguzi
Upande wenye uthubutu na maamuzi
Upande wenye machozi jasho na damu
Uongozi upako ufahamu, upande usio na uhuru na uchaguzi

Upande uliofanya wanaume tutengwe na tunu
Tutengwe na tunu
Upande ambao pengine kuishi wewe ni ngumu
Upande ambao asali yake ni kilele cha sumu

Upande ambao haushabikii tija ya upendo au furaha au amani
Kama hauangalii pima utagundua upande niliosimama mimi ni ngao ya jamii nzima

Uanaume sio ushindi ni jukumu
Uanaume sio rizki ni hukumu
Ungejua kwanini wanaume wana msongo wa mawazo pengine ungefurahia udogo wako

Dear women , dear girls

Mmekuwa chombo cha ngono
Maana mmetufanya chombo cha fedha
Kama nguo hazitabadili mishono
Hatuwezi kuwa marafiki bila ngono nawaeleza

Mnapoona padogo pana taswira ndefu
Kiasi haujui si ndio tuliopigana vita yenu
Hata mkiamka mmekuwa wanaume leo
Mtagundua kuwa jinsia sio cheo

Wapendwa tukishindana mtashindwa
Hata mkishinda ushindi wenu hautalindwa
Kama ambavyo kila mmoja anatumia choo chake
Kila mmoja a-play role yake na awe bingwa

Dear women

Ndoa sio mafanikio
Kuna wengi wanakonda maana ndoa zao sio
Ndoa ni mwiba usijivune
Ukiipata niamini unaweza kukamilika bila mume

Dada baki shule bila elimu utateseka
Ukitegemea urembo ipo siku utazeeka
Kama ukiweka mwili wako hisani
Ukizeeka tutajali ulichonacho kichwani

‘Skiza’ hata wanaume tuna doubts too
And this world doesn’t revolve around you
Tuna stress zinatufunga na tena
Kazi zetu ni ngumu ndo’ maana tunakufa mapema

Kama unahisi upo huru umepotoka
Hauwezi kuwa huru wakati umelipiwa posa

Dear women

It’s okay kuwa namba mbili
Majukumu sio mashindano acha kukalili

It’s okay kumlea mwanaume asiye na kazi
Ukaendelea kumuheshimu bila kumshusha hadhi
Mbona sisi tunalea wanawake masikini wamekata ringi na bado mtaani hatutatangazi

Mwanaume ana jukumu la kujenga msingi?
No, msingi unajengwa na elimu
Kwa mfano nani anayekubali kucheza uchi kwenye videos? Jiheshimu nikuheshimu

Urembo pia ni power, ila ni power na iogope
Maana ni upanga unaokata pande zote
Ngoma ya uzuri haitovuma milele
Ukiutumia urembo vibaya utakuvunja mwenyewe

I wish ungejua unachowaza ni muhimu
Ukifanyia kazi na kuwa wa kwanza si’ majibu
I wish ungejua kwamba asili imenipa umwamba
Nikulee, kukulea wewe ni msaada si’ wajibu

I wish ungejua tuko tofauti hata utunge dini
Hauwi mwamba kwa kumweka mwanaume chini
I wish ungejua kuwa kichwa ni hukumu
Maana hakuna kinachotisha kama jukumu

Wangapi tumelelewa na hao single mothers
Maskini and we turned out just fine
Maybe idea ya kuacha kujali mtoto sababu
Baba mjinga ingeachwa far behind

Tunasubiria uhalisi ubadilike
Labda uhalisia haubadiliki huu
Labda ni wakati wa kukubali ili yaishe kwamba
Mtoto ni wa mama na baba ni rafiki tu

Lini mtaacha kutuita madanga ma-sponsors? Ndio, niheshimu nikuheshimu nitaacha wewe
Ukiona imetosha, au sio?

Najua tuko tofauti
Na tofauti itabaki hivyo milele
Usinichukie nielewe

Dear girls, dear women

Ni sisi kina kaka kina baba, wanaume machizi wenu
Tunawasilisha kutoka upande wa juu, upande mbali uliowekwa na asili yetu

( Dizasta Vina )
www.ChordsAZ.com

TAGS :