Song: 2025
Artist:  Shark D
Year: 2021
Viewed: 60 - Published at: 4 years ago

Nikama ndoto kumbe ukweli umeondoka
Umepigana vita kali mabepali wakaondoka
Hukuogopa kuyasema ya moyoni
Tanzania imepata pengo kuliziba ni kama skendo

Tuliamini chato itatoboa wilaya mpaka mkoa
Ila leo wanaisodoa pia wanaitia doa
Ulivyolala wameilaza kilichobaki nikuisambaza
Madini wakapiga uliowaamini kwenye siasa

Umeondoka we jasili wanakuponda bila siri
Uongozi umevurugwa wanakusinichi uliowaamini
Uliowatoa kwenye kazi wamerudishwa na mwendo kasi
Ni madaraka yaliyo wazi yasiyoheshimu hata wazazi

Siogopi kusukuma kusukumwa na Msukuma
Dunia hairudi nyuma cha msingi ni kukaza chuma
Chuma kimeshalala na wengine ndio wanavuma
Chuma kimeshalala mipango yote ndio inabuma

Pole mweshimiwa Bashiru katibu mpaka mbunge
Siasa ya kinyonge piga kazi we usikonde
Tulikwamini kama jasili uliyepigana kwa akili
Leo wamekuona huna akili wamekushusha mpaka chini
Tanzania ya viwanda leo imegeuzwa karanga
Inaongozwa na wajanja wanaopanga na kusaga
Siasa haina dili mchapakazi hana dili
Wanaopangwa kwenye kazi wana mbinu za ujangili

Walio sema vyuma vimekaza leo salamu wameipata
Tanzania hakuna bata tuna enjoy tunachopata
Eyo family punguza tapatapa
Mother kashasema round hii tutaipata

Awamu imekuwa ngumu kutishana na majukumu
Mkubwa kaweka ngumu kupumua nikama pumu
Ukizingua anazingua ndio kauli ya kusitua
Na wananchi wanapumua huku wameziba pua

Mawaziri fake wamerudishwa kudadeki
Tutapiga deki bahari ya hindi kama washenzi
Watoto wamevaa nepi wakubwa ndani ya net
Siasa ya vyama vingi imefutwa kudadeki

Wanasema mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni
Tukutane 25 kwenye foleni za kampeni
Tufute madeni au turudi kwenye deni
Ndio dalili zinazoonesha tunarudi sebureni

( Shark D )
www.ChordsAZ.com

TAGS :