Song: Elimu Dunia
Artist:  Daz Baba
Year: 2004
Viewed: 47 - Published at: 9 years ago

[Instrumentals]
Verse 1:
Fikra za ajabu, kiburi pamoja na zogo
Nilionekana nnazo tangu nikiwa mdogo
Michezo ya hatari, pamoja na dhuluma
Kiburi kwa wakubwa zangu walipo nituma
Ndipo wazazi wangu walikaa chini wakafikiri, japokuwa mimi mkubwa' nianze skuli
Ndipo nilipoanza la kwanza mpaka la pili’ ambapo kamari na jeuri vikawa vimeshamiri
Nikasogea sogea mpaka darasa la tatu, hapo nikazidi kuikata elimu katu katu
Maombi ya wazazi na "Mswalie,mswalie, Mtume"' ndivyo vilivyonisaidia mi kufika la nne
Ambapo nkakataa shule, nikawa nipo zangu tu maskani, huku niki tathmini mali za majirani
Leo nikavunje pale' kwa tajiri fulani, ili mradi tu nipate chochote kinywani
Hakika nilifanya kila aina ya unyama
Ofisi yangu ufunguliwa jua lilipozama
Nnacho kumbuka Mama yangu alilia sana, hata Baba katishia kuniachia laana...
Chorus:
Elimu Dunia’ mwenzenu nilikataa...
Elimu Dunia' mwenzenu nilikataa...
Nilipenda maasi' nimekumbwa na balaa...
Maisha yangu yote naishia mfungwa...
Elimu Dunia' mwenzenu nilikataa...
Mwenzenu nilikataa...
Nilipenda maasi' nimekumbwa na balaa...
Maisha yangu yote naishia mfungwa...
Elimu Dunia'
Verse 2:
Wash'kaji walikuwa wakija nigongea night kali
Kamanda amka, tuende tukausake utajiri
Hata kwa njia zile' ambazo sio halali’ nikakubali, ni kawa silali
Nafanya vile akili yangu ilivyonituma
Navunja mlango hata kwa Jiwe Fatuma
Yeyote aliyeleta ubishi kutoa mali, alitolewa uhai, nlichokuwa nkitaka kwake kwanza ni masilahi
Maasi yangu mwisho yakaongezeka, habari kwenye vyombo vya dola kote zikafika, matangazo kwenye magazeti sasa yakaandikwa
Jambazi muhalifu’ anatafutwa, na donge nono litatolewa endapo atakamatwa
Hauwezi kuamini kweli arobaini zake mwizi' siku hiyo kwenye kazi nimenasa kitanzi...
Naishia gerezani...
Chorus:
Elimu Dunia’ mwenzenu nilikataa...
Elimu Dunia' mwenzenu nilikataa...
Nilipenda maasi' nimekumbwa na balaa...
Maisha yangu yote naishia mfungwa...
Elimu Dunia' mwenzenu nilikataa...
Mwenzenu nilikataa...
Nilipenda maasi’ nimekumbwa na balaa...
Maisha yangu yote naishia mfungwa...
Elimu Dunia'
Verse 3: Afande Sele
We ni mfungwa sasa' si mtu huru
Ukilalamika sana utakuwa kama unakufuru' tu
Lazima ujue' sisi ni vifaranga na maisha ni kama mwewe
Mama yetu ni elimu, ulio mkataaga we mwenyewe' zamani
Ulimkataa elimu ya duniani, ukampiga hadi mwalimu' darasani
Ukusikia la Muadhin wala la Mnadi swala hukuliamini
Umri ulikudanganya, ukawa mbabe shuleni' sasa ndo hivyo uko nasi gerezani
Jiamini mdogo wangu, kwani jela sio kaburini au kwa Mungu
Umetengwa na jamii, hujatengwa na dunia hii
Jifunze kupokea furaha sawa na huzuni
Kumbuka kwamba taabu na raha zipo duniani, zipo kwa ajili ya watu na watu' ndio mimi na wewe
Kila mmoja atabeba madhambi yake mwenyewe' imeandikwa
Kama umekunywa sumu, sasa ya nini uombewe? Eh, sasa ya nini uombewe?
Ah!
Hook:
Yay,yay,yay,yay,yo...
Oh hoo.. yay,yo...
Nime waharibia hadi ndugu na jamaa, nimekosa hata wakuniwekea dhamana
Ndege mjanja asie naswa, nimeishia ukingoni
Mabawa yamekatika, mwokozi mi simwoni
Uraiani kurudi sidhani...
Daz Nundaz, Scout Jentaz, Sewa Side
Tamaa zilinifanya niwe gaidi, fikra zangu ulimwengu nita umudu
Leo unanifunza kwa mola na tubu, Ya maulana' niokoe kwenye gharika, mja wako unitoe
Leo ndio usemi umetimia... hauna kilio msiba wa kujitakia
Chorus:
Elimu Dunia' mwenzenu nilikataa...
Elimu Dunia' mwenzenu nilikataa...
Nilipenda maasi' nimekumbwa na balaa...
Maisha yangu yote naishia mfungwa...
Elimu Dunia' mwenzenu nilikataa...
Mwenzenu nilikataa...
Nilipenda maasi' nimekumbwa na balaa...
Maisha yangu yote naishia mfungwa...
Elimu Dunia'
[Instrumentals]

( Daz Baba )
www.ChordsAZ.com

TAGS :