Song: Mwaka Wangu
Artist:  Harmonize
Year: 2022
Viewed: 38 - Published at: 9 years ago

[Intro]
Yaw-yaw
Jeshii
La-la-li-la-la, mmh, la-la-la
Chiiii
Eeh

[Verse 1]
Ni mwaka mpya mambo mapya sina dhambi nimetubu
Na pesa ntazichanga change nizijaze kwa kibubuu
Japo hata kakibanda nikajenge huko pugu
Maana nyumba za kupanga nishazichoka vurugu
Eti kwani wao waweze wana nini (Mmmh)
Na mimi nishindwe nina nini
Nishachoka siku zote kuwa wa chini
Wengine wanakula kipupwe ma ofisini

[Pre-Chorus]
Mliosema haolewi olewi mbona kaolewa
Mliosema hapewi hapewi mbona amepewa
[Chorus]
Mwaka huu ni wangu kutimiza ndoto zangu
Nasema mwaka huu ni wangu kwa baraka za mungu wangu, dear Lord
Hakuna mungu kama wewe babaa (Eh, hakuna)
Kama wewe yawee (Eh, hakuna)
Hakuna mungu kama wewe babaa (Eh, hakuna)
Kama wewe yawee (Eh, hakuna)

[Verse 2]
Huu mwaka nakusanya mavumba ninunue gari yangu
Na wale waliosema mimi ni mguma waje wamuone mwanangu
Huu mwaka marafiki wasio na faida nawaweka pembeni
Wanaokufata wakati wa shida ili wapate hafueni
Niwaonyeshe walionidharau kama mungu anaweza
Nami nipande dau niwasalimu kingereza

[Bridge]
When God say yes nobody can say no
(When God say yes nobody can say no)
When God say yes nobody can say no
(When God say yes nobody can say no)

[Pre-Chorus]
Mliosema haolewi olewi mbona kaolewa
Mliosema hapewi hapewi mbona amepewa
[Chorus]
Mwaka huu ni wangu kutimiza ndoto zangu
Nasema mwaka huu ni wangu kwa baraka za mungu wangu, dear Lord
Hakuna mungu kama wewe babaa (Eh, hakuna)
Kama wewe yawee (Eh, hakuna)
Hakuna mungu kama wewe babaa (Eh, hakuna)
Kama wewe yawee (Eh, hakuna)

( Harmonize )
www.ChordsAZ.com

TAGS :