Song: Nimekubali
Artist:  Ibraah
Year: 2020
Viewed: 34 - Published at: 9 years ago

[Paroles de "Nimekubali"]

Kapipo on the beat, hey eeeh
Ooh nanana, ooh mamama
Maulana mmmh

(Kapipo)

Kapu limeshajaa
Mapitilizo maudhi yamezidi
Moyo wangu uko mbali nawe

Soko la karafuu umeuza dagaa
Na ule utamu umeugawia kijiji
Umenipa donda la roho
Isipagawe

Mungu amenipa ufahamu
Natambua lipi chema na baya
Usizuge kwa tabasamu
Kumbe huna lako moyoni
Na nishazoea mila
Kikwetu kusema sema ni roho mbaya
Ningalikuwa na uwezo
Mwanzo ningekuficha mfukoni

Ulinidanganya kumbi kumbi
Nilale bila chandarua
Kumbe mbu nang'ata

Si ulinikung'uta mavumbi
Nilipo omba nyingi dua
Ukaniondolea mashaka

Mapenzi hayalazimishwi
Haukuridhiana na mimi nenda
Ila nakuombea
Ukaishi maisha mema

Pia siwezi na silazimishi
Labda sina dhamani, huenda
Kuondoka kwako kwangu
Mungu akaleta mema

Nimekubali mimi, japo ni maumivu ila
Nimekubali mimi, japo hutoki kwa akili yangu unaizunguka
Nimekubali mimi, nimekubaliana na wewe eeh
Nimekubali mimi, nimekubaliana na weee
Japo ni ngumu ka imenikwama miiba
Maana kwa ndani ndani bado inanichoma
Na maumivu huwezi yasikia
Nayasikia mwenyewe tu

Na hali ya upweke sio kawaida
Najua dhahiri kuwa na kinyima amani
Stress ingekuwa kilevi
Ndio kulala na viatu

Jua mwana ukiyataka ndo mwana kuyapata
Mungu hamnyimi mja wake
Usinung'unike kwa utakacho kipata
Maana ndo unachotafuta

Umekuwa gari la taka, haunaga tabaka
Umekosa hadhi ya mwanamke
Tulia yakufuate magari bovu
Ndo kutwa ukafuata fuata wee

Mapenzi hayalazimishwi
Haukuridhiana na mimi nenda
Ila nakuombea
Ukaishi maisha mema

Pia siwezi na silazimishi
Labda sina dhamani, huenda
Kuondoka kwako kwangu
Mungu akaleta mema
Nimekubali mimi, japo ni maumivu ila
Nimekubali mimi, japo hutoki kwa akili yangu unaizunguka
Nimekubali mimi, nimekubaliana na wewe eeh
Nimekubali mimi, nimekubaliana na weee

( Ibraah )
www.ChordsAZ.com

TAGS :