Song: Sawa
Artist:  Ibraah
Year: 2020
Viewed: 40 - Published at: 4 years ago

[Paroles de "Sawa"]

It's Bonga
(Oh nah nah nah nah nah aah)

Asante Mungu Baba uliye mwema
Nimeiona siku nyingine ya furaha
Hali sio haba sio njema
Wa kuniponya nipate hata chembe ya furaha

Maana wazazi wananitegemea
Na ninakaribia mi kuitwa Baba
Nami ndunguzo waloegemea
Sina kitu nimechalala nimevava

Uniepushe mabaya dunia
Yasijenikumba
Napiga goti kwa uchungu nalia
Ni nusuru muumba

Katu nisikate tamaa
Niende kusaka tonge
Nipate ama nishinde njaa
Moyoni upige konde, ni sawa eh!
Ni sawa, ni sawa
Nami nitafika (Ata nikikosa sawa)
Ni sawa, ni sawa
Nami mimi utanipa (Ah ridhiki we ndo unayegawa)

Sawa, ni sawa
Nami nitafika (Mwanadamu hawezi panga)
Ni sawa, ni sawa
Nami mimi utanipa (Sitozuguka kwa waganga)

Natapa tapa elimu sina
Mi kusoma sijasoma
Nami nasaka nijenge heshima
Mi nakoma ju wananichoma

Ni wewe pekee ndo naye jua
Ah mbele yangu na nyuma yangu
Mie mpweke naomba dua
Ah Baba fungua ridhiki zangu

Nashukuru Baba, pumzi unayonipa
Maisha naendelea
Ila kingine Baba, nadhalilika
Huu mzigo unanielemea

Baba niwewe Baba (Ni wewe)
Niwe ndo msaada (Ni wewe)
Ni wewe, ni wewe
Baba ni wewe
Uniepushe mabaya dunia
Yasijenikumba
Napiga goti kwa uchungu nalia
Ni nusuru muumba

Katu sikate tamaa
Niende kusaka tonge
Nipate ama nishinde njaa
Moyoni upige konde

Ni sawa, ni sawa
Nami nitafika (Ata nikikosa sawa)
Ni sawa, ni sawa
Nami mimi utanipa (Ah ridhiki we ndo unayegawa)

Sawa, ni sawa
Nami nitafika (Mwanadamu hawezi panga)
Ni sawa, ni sawa
Nami mimi utanipa (Sitozuguka kwa waganga)

( Ibraah )
www.ChordsAZ.com

TAGS :