Song: Unavyofanya
Artist:  Daz Baba
Year: 2004
Viewed: 50 - Published at: 4 years ago

Chorus: Daz Baba
Unavyofanya sivyo' watu watakuona ovyo...
Tabia yako sio' maishani utapata matatizo...
Matatizo!...
Asa kwanini ufanye hivyo' wakati unajua sivyo...
Tabia yako sio' kwenye jamii utaleta matatizo...
Matatizo!...

Verse 1:
Mwingi wa kukopa' kulipa matanga, shida kidogo unakwenda kwa waganga
Mwingi wa kukopa' kulipa matanga, shida kidogo una kimbilia kwa waganga
Kuwa tesa yatima unaona inalipa, hutaki kutumia hekima mola alizokupa...
Unapo ishi kila mtu akuchukia' mwingi wa habari na mchafu kitabia>>Kitabia
Umesahau sasa kazi>>Kazi, unacho endekeza pombe na mapenzi>>Mapenzi
Na'
Umepuuza ya wazazi' unachofanya ni ushenzi, ushenzi...

Chorus:
Unavyofanya sivyo' watu watakuona ovyo...
Tabia yako sio' maishani utapata matatizo...
Matatizo!...
Asa kwanini ufanye hivyo' wakati unajua sivyo...
Tabia yako sio' kwenye jamii utaleta matatizo...
Matatizo!...
Verse 2:
(?) unajifanya usikii, kuna magonjwa ya zinaa
Ngono unaongeza bidii, jamaa ana wakemea, tena wana kosea, wewe unawatetea' badili hiyo tabia...
Pia ukilewa' una itelekeza hadi yako familia...
Hivi wewe Muumini mzima' una msaliti hadi Mungu...
Dini yake moja' unaiweka ki mafungu...
Akati Mungu ni yulе yule mmoja' na watu wake wote tunakwеnda sehemu moja...

Chorus:
Unavyofanya sivyo' watu watakuona ovyo...
Tabia yako sio' maishani utapata matatizo...
Matatizo!...
Asa kwanini ufanye hivyo' wakati unajua sivyo...
Tabia yako sio' kwenye jamii utaleta matatizo...
Matatizo!...

Verse 3:
Pande zote una sifika kwa udokozi, badala ya ku make deal' unaleta ubitozi
Taka una toa home, unatawanya mitaani, badala ya kwenda msalani unajisaidia vichochoroni
Asa mazingira yata safishwa na nani...?
Mbona unavibweka kama katuni wa Sani
Na' unavyofanya how come ukilewa una beba demu hukumbuki tena kondomu, wakati mtu muhimu
Tutakuita marehemu'
Tutakuita marehemu...

Chorus:
Unavyofanya sivyo' watu watakuona ovyo...
Tabia yako sio' maishani utapata matatizo...
Matatizo!...
Asa kwanini ufanye hivyo' wakati unajua sivyo...
Tabia yako sio' kwenye jamii utaleta matatizo...
Matatizo!...
[Instrumentals]

( Daz Baba )
www.ChordsAZ.com

TAGS :