Song: Lissa 2
Artist:  Rapcha
Year: 2021
Viewed: 42 - Published at: 8 years ago

Eugen sogea karibu kidogo

Kabla sijakata pumzi ya mwisho tuongee japo kidogo

Enjoy kila siku iendayo kwa Mungu

Kwenye maisha ya mwanadamu siku za furaha huwa ni ndogo

Sijapanga kumkufuru muumba

Ila kwa leo tu ningemuomba arudishe tu masaa nyuma

Haya mateso nnayopata kwenye hiki kitanda
Damu yangu itamlilia Lissa haitokaa kimya

Mwambie asichelewe nitamsubiri paradiso

Kama nitapona Basi sitomsahau mpaka kifo

Kumbukumbu zitamfata kila unyayo
Amekatisha ndoto yangu kubwa nlionayo

Najua Kabla hawajatangaza misa

Millard Ayo, Sam Misago, Simulizi watauliza Kisa

We waambie mi ilikuwa nije niwe namba Moja

Ila mtu mmoja tu ndoto yangu ameikatisha

Eugen Najua mama yangu atalia

Atanimiss kila siku na atakua anaumia

Alitamani niwe padri nkaona mziki unanihitaji

Usiache kumsalimu home

Mpe na pesa ya mahitaji

Mwambie mama sikuacha sala

Ugumu wa pesa ndo umefanya nshindwe kuja home kila mara

Pesa inatesa vibaya
Na ukiiweka mbele kabla ya Mungu ndio mwanzo wa ubaya

Hii habari itamuumiza Majani

Plan zetu zote kubwa zimeishia njiani

Lile Gari aliloniagizia ampe mama

Priscus atamfunza ku-drive ataenda Nalo kanisani

Mwambie father atalipwa na mola

Arudishe moyo nyuma amsamehe Paula

Mwambie alinitimizia ndoto kunisign bongo records

Wengi walinikataa ye akaona nyota inayong'ara

Mziki umeniintroduce kwenye maisha ambayo ngumu Sana kumpata mpenzi aliesahihi

Katika kuendelea kumtafuta ndo nkajikuta
Naongeza list wanachuo mpaka wasanii

Kwangu alikosa kipi

Akaamua aache siti kubwa nliyompa kwenye moyo akadandie lift
Nlitulia ingawa wanawake wanaamini kuwa mwanaume hata akikupenda vipi lazma atakucheat

Ntakua mgeni wa nani

Mara ngapi jumapili nilitii wito wako nkaacha kwenda kanisani

Leo nakufa kitandani

Vilivyonifanya mpaka nikawa mbali na Mungu wangu sivioni

Kupeana mapresha tu

Kwenye mapenzi watu hawaumizi expectations do

Wengine walitamba haikupita hata mwezi tu
Sasaivi wako busy Wanafuta tattoo

Kama ikitokea nkapona sitofanya revenge

Awe na amani maana amechagua maisha ya kutrend

Wala msimchukie maana kila mtu ana mabaya yake

Tunaact tuko perfect tunapretend

Unahisi,Ngoma zitaendelea kupigwa radio?

Nlitamani nipate tuzo Zaidi ya pesa ya nguo

Mama angu Jide ataumizwa Sana na hii habari

Mwambie asante kwa kunishika mkono hii safari

Utaniagia mashabiki

Waliozimia Ngoma zangu ndani na nje ya nchi

Inawezekana mziki bila kiki

Ila kiki ni kama madawa ukiyatumia hauachi

Wanangu nawatakia maisha marefu

Ka tutaonana baadae tutaongea kwa kirefu

Wakumbushe bysa na chatta watafute tu cash

Coz you stop living when you stop believing in yourself

Asante kwa kunisikiliza naitwa Rapcha

Last king of 90’s baby

( Rapcha )
www.ChordsAZ.com

TAGS :