Song: Lissa
Artist:  Rapcha
Year: 2021
Viewed: 35 - Published at: 8 years ago

Saa Sita Mchana jua la utosi

Chuo Boom limetema Nimekaa Kibosi hata presha ya msosi sina

Prr somebody's calling, Ooh Kumbe Lissa
Nimemsave Love Of My Life

Nkaweka Na Loud speaker

Nkamsikia Anaongea Ka Analia Nkamuuliza are you okay Monalisa??

Akaniambia

Baby siko sawa kabisa

Nadaiwa Ada Na Jumatatu ndo tunaanza paper yani

Na nisipolipa siruhusiwi kufanya mitihani

Laki 5 nzima ntaitoa wapi honey!?
Ouhh Don Worry Nalifix Boo

Kwakuwa Nishadaka hela ya boom Nkalibeba hilo jukumu

Nkamwambia basi nakutumia

Usikate Simu Kwanza love ili uniambie ikiingia

Mh Baby Mbona hii namba Ina jina la kiume'?

Akanambia hiyo line ni kaka ake alimsajilia


Laki 5 kwenda kwa Lissa Bonyeza 1 kuthibisha 2 kubatilisha mi nkathibitsha

Laki Tano na elfu 5 ya makato ya kutoa kwenye akaunti yake palepale ikathibitishwa

She was like thanks baby nimeiona

Jioni jua likipoa Nitakuja kwako kukuona

And for real nmekumiss kinoma

Nkamwambia nitafurahi Sana kama nitakuona

Saa kumi na moja mtoto hajatimba
Labda ndo anatoka home acha nvunge mida mida anafika

Saa moja kamili mtoto hajatimba.. nkasema huenda foleni kubwa ila punde tu atafika

Saa tatu usiku mtoto hajatimba giza limetinga

Nshampigia Sana simu hapokei text zinadunda

Nkawaza mpaka usingizi ukanichukua

Siku ya pili simu hapokei text hajafungua

Siku ya tatu kimya nikasanuka nicheck best yake huwezi amini nilijuta kumpigia

Nkamwambia hey shem you good !?

I'm good

Siku ya tatu best yako ka nlia buyu

Nowdays Lissa mbona ana ma drama huyu

Akanambia shem Kama unakifua ntakuambia

Kweli Lissa amechange
Ana bwana mpya Msanii huyo ndo anaemdrive crazy

Juzi Si ulitumia hela ya Ada alipokulilia

Hiyo hela kampa bwanaake akatumia

Maumivu huwa makali ukimpa kitu mtu

Umpendae akampatia ampendae zaidi

Magoti yaliniisha nguvu chozi chini mbupu ndichi

Roho Iliniuma kinoma sikufichi

Nkaondoka Home Kwa Hasira

Nimfate Lissa coz jealous inanitesa na kila

Nkimuwaza naona ka Dereva anautani na mimi

Daladala nliona inaenda taratibu nlitamani nkaiendeshe Mimi

Nkafika Mpaka Kwa Lissa

Ile Naukaribia Mlango Naskia Mziki Ila Kuna sauti ka sizielewi

Nkaona siwezi gonga mlango

Nkapita nao na teke mpaka ndani nlichokiona sitosahau maishani

Kidume kinamkazia kitanda ndani

Ye busy Analia machozi hayatoki anaifinyia ndani

Hata hawakushtuka wamuhofie Nani

Jamaa akapiga tako 8 akamwagia ndani

Nlipatwa kizunguzungu nusu nianguke sikuweza kuamini

Lissa Mbona umenitenda hivi nmekukosea Nini

Ungeniambia tuachane ningekuacha huru

Mwisho wa siku ningepona sasa haya yote ya nini

Lissa akanibadilikia sura mpaka sauti amanichenjia

Akaanza kunitimua huku na matusi ananishushia

Yeye na Bwanaake wAkanipush mpaka nje

Akanipigia kelele ya mwizi watu akanijazia

Watu wakanijalia wameshika mawe na marungu

Wakanipiga Kama mwizi huo mtaa sina ndugu

Hakuna wa kunitetea

Wakanivika tairi ya Gari wakawasha Moto fasta nkaanza teketea

Maumivu ya moto ndo haya

Walioniunguza moyo wameuteketeza na mwili vibaya

Nna sekunde chache za kuivuta pumzi ya dunia nzuri iliyojaa binadamu wengi wabaya

Sawa Lissa Ninakuacha ufurahi

Mapenzi nliyokuonesha umeamua kunitoa uhai

Ahadi tulizoweka zimezimwa na tamaa zako

Mi nakwenda, Karma itakulipa bye bye

( Rapcha )
www.ChordsAZ.com

TAGS :