Song: Usihukumu
Artist:  Daz Baba
Year: 2004
Viewed: 48 - Published at: 9 years ago

[Instrumentals]

Chorus:
Usi hukumu mwenzako bila ya kujua, utakuwa unakosea
Disa' kwani wote tumeletwa na mwenyezi' chini ya jua
Sure' ah...aah...aahaa...
( Watu wanaishi vipi )
Bora ukinielewa...
( Maisha mafupi )

Verse 1:
Ukisikia' kwanza fuatilia, ukishajua Ndipo uchukue hatua
Usipende kuhisi zaidi ya kudadisi, haifai kumuita mtu wa mola, ibilisi
Masela wangu wapo' jela kitambo, wanalalamika uswazi hawajafanya mambo
Hawajui lini milango itafunguka, wasio na hatia waweze toka
Adui au rafiki hadi sasa hajulikani, vipi mwanadamu achukue sheria mikononi
Hata tukiulizana yupi anaeongoza kwa mema, usiku na mchana tutakesha' hatutamuona

Chorus:
Usi hukumu mwenzako bila ya kujua, utakuwa unakosea
Disa' kwani wote tumeletwa na mwenyezi' chini ya jua
Sure' ah...aah...aahaa...
( Watu wanaishi vipi )
Bora ukinielewa...
( Maisha mafupi )
Verse 2:
Wote tumezaliwa' dunia tumeikuta, yote hatutaimaliza, tupo njiani tunapita
Usimdharau yule usiyemjua kwani baadaе anaweza akakusaidia
Usimhukumu yeyote yulе' kwa ajili ya mavazi yake
Usimshutumu yeyote yule' kwasababu ya makazi yake
Kama mmekoseana mueleweshane, isiwe sababu mbali mfikishane
Maisha ni matamu lakini ni mafupi, na wote hatujui hukumu yetu saa ngapi

Chorus:
Usi hukumu mwenzako bila ya kujua, utakuwa unakosea
Disa' kwani wote tumeletwa na mwenyezi' chini ya jua
Sure' ah...aah...aahaa...
( Watu wanaishi vipi )
Bora ukinielewa...
( Maisha mafupi )

Outro:
Tusihukumu wachanga, yeah! Hawajui wanapo kwenda
Un-huh!
Daz Nundaz, Sewa Side, (?) , Majani, tufate haki, ausio?
Yeah, Mon!

[Instrumentals]

( Daz Baba )
www.ChordsAZ.com

TAGS :